| Chapter 17 |
1 |
Kisha, Yesu akawaambia wanafunzi wake, "Haiwezekani kabisa kusitokee vikwazo vinavyosababisha dhambi; lakini ole wake mtu yule atakayevisababisha. |
2 |
Ingekuwa afadhali kwake kufungiwa shingoni jiwe kubwa la kusagia na kutoswa baharini, kuliko kumkwaza mmoja wa wadogo hawa. |
3 |
Jihadharini! Kama ndugu yako akikukosea, mwonye; akitubu, msamehe. |
4 |
Na kama akikukosea mara saba kwa siku, na kila mara akarudi kwako akisema `Nimetubu`, lazima umsamehe." |
5 |
Mitume wakamwambia Bwana, "Utuongezee imani." |
6 |
Naye Bwana akajibu, "Kama imani yenu ingekuwa ndogo hata kama chembe ndogo ya haradali, mngeweza kuuambia mti huu wa mkuyu: `Ng`oka ukajipandikize baharini`, nao ungewatii. |
7 |
"Tuseme mmoja wenu ana mtumishi ambaye analima shambani au anachunga kondoo. Je, anaporudi kutoka shambani, atamwambia: `Haraka, njoo ule chakula?` |
8 |
La! Atamwambia: `Nitayarishie chakula, ujifunge tayari kunitumikia mpaka nitakapomaliza kula na kunywa, ndipo nawe ule na unywe.` |
9 |
Je utamshukuru huyo mtumishi kwa sababu ametimiza aliyoamriwa? |
10 |
Hali kadhalika na ninyi mkisha fanya yote mliyoamriwa, semeni: `Sisi ni watumishi tusio na faida, tumetimiza tu yale tuliyotakiwa kufanya."` |
11 |
Yesu akiwa safarini kwenda Yerusalemu alipitia mipakani mwa Samaria na Galilaya. |
12 |
Alipokuwa anaingia katika kijiji kimoja, watu kumi wenye ukoma walikutana naye, wakasimama kwa mbali. |
13 |
Wakapaza sauti wakisema, "Yesu Mwalimu, tuonee huruma!" |
14 |
Alipowaona akawaambia, "Nendeni mkajionyeshe kwa makuhani." Basi, ikawa walipokuwa wanakwenda, wakatakasika. |
15 |
Mmoja wao alipoona kwamba ameponywa alirudi akimtukuza Mungu kwa sauti kubwa. |
16 |
Akajitupa chini mbele ya miguu ya Yesu huku akimshukuru. Huyo alikuwa Msamaria. |
17 |
Hapo Yesu akasema, "Je, si watu kumi walitakaswa? Wale tisa wako wapi? |
18 |
Hakupatikana mwingine aliyerudi kumtukuza Mungu ila tu huyu mgeni?" |
19 |
Halafu akamwambia huyo mtu, "Simama, uende zako; imani yako imekuponya." |
20 |
Wakati mmoja, Mafarisayo walimwuliza Yesu, "Ufalme wa Mungu utakuja lini?" Naye akawajibu, "Ufalme wa Mungu hauji kwa namna itakayoweza kuonekana. |
21 |
Wala hakuna atakayeweza kusema, `Uko hapa`, au `Uko pale`. Kwa kweli Ufalme wa Mungu uko kati yenu." |
22 |
Halafu akawaambia wanafunzi wake, "Siku zinakuja ambapo mtatamani kuona mojawapo ya siku za Mwana wa Mtu, lakini hamtaiona. |
23 |
Na watu watawaambieni: `Tazameni yuko hapa`; ninyi msitoke wala msiwafuate. |
24 |
Kwa maana kama vile umeme unavyotokea ghafla na kuangaza anga upande mmoja hadi mwingine, ndivyo Mwana wa Mtu atakavyokuwa siku yake. |
25 |
Lakini kabla ya hayo, itambidi ateseke sana na kukataliwa na kizazi hiki. |
26 |
Kama ilivyokuwa nyakati za Noa, ndivyo itakavyokuwa katika siku za Mwana wa Mtu. |
27 |
Watu waliendelea kula na kunywa, kuoa na kuolewa mpaka wakati ule Noa alipoingia katika safina. Gharika ikatokea na kuwaangamiza wote. |
28 |
Itakuwa kama ilivyotokea wakati wa Loti. Watu waliendelea kula na kunywa, kununua na kuuza, kupanda mbegu na kujenga. |
29 |
Lakini siku ile Loti alipoondoka Sodoma, moto na kiberiti vikanyesha kama mvua kutoka mbinguni na kuwaangamiza wote. |
30 |
Ndivyo itakavyokuwa siku ile Mwana wa Mtu atakapofunuliwa. |
31 |
"Siku hiyo, yeyote atakayekuwa juu ya paa asishuke nyumbani kuchukua mali yake. Kadhalika, naye atakayekuwa shambani asirudi nyuma. |
32 |
Kumbukeni yaliyompata mke wa Loti. |
33 |
Yeyote anayetaka kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na yeyote anayeipoteza, ataiokoa. |
34 |
Nawaambieni, siku ile usiku watu wawili watakuwa wanalala pamoja, mmoja atachukuliwa na yule mwingine ataachwa. |
35 |
Wanawake wawili watakuwa wakisaga nafaka pamoja; mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa."*fc* atachukuliwa na mwingine ataachwa.\ie |
36 |
missing |
37 |
Hapo wakamwuliza, "Ni wapi Bwana?" Naye akawaambia, "Ulipo mzoga, ndipo tai watakapokusanyikia." |