| Chapter 16 |
1 |
Sasa, yahusu ule mchango kwa ajili ya watu wa Mungu: fanyeni kama nilivyoyaagiza makanisa ya Galatia. |
2 |
Kila Jumapili kila mmoja wenu atenge kiasi cha fedha kadiri ya mapato yake, ili kusiwe na haja ya kufanya mchango wakati nitakapokuja. |
3 |
Wakati nitakapokuja kwenu, nitawatuma wale mtakaowachagua miongoni mwenu wapeleke barua na zawadi zenu Yerusalemu. |
4 |
Kama itafaa nami niende, basi, watakwenda pamoja nami. |
5 |
Nitakuja kwenu, baada ya kupitia Makedonia--maana nataraji kupitia Makedonia. |
6 |
Labda nitakaa kwenu kwa muda fulani, au huenda nitakaa pamoja nanyi wakati wote wa baridi, ili mpate kunisaidia niendelee na safari yangu kokote nitakakokwenda. |
7 |
Sipendi kupita kwenu harakaharaka na kuendelea na safari. Natumaini kukaa kwenu kwa kitambo fulani, Bwana akiniruhusu. |
8 |
Lakini nitabaki hapa Efeso mpaka siku ya Pentekoste. |
9 |
Mlango uko wazi kabisa kwa ajili ya kazi yangu muhimu hapa, ingawa wapinzani nao ni wengi. |
10 |
Timotheo akija, angalieni asiwe na hofu yoyote wakati yupo kati yenu, kwani anafanya kazi ya Bwana kama mimi. |
11 |
Kwa hiyo mtu yeyote asimdharau, ila msaidieni aendelee na safari yake kwa amani ili aweze kurudi kwangu, maana mimi namngojea pamoja na ndugu zetu. |
12 |
Kuhusu ndugu Apolo, nimemsihi sana aje kwenu pamoja na ndugu wengine, lakini hapendelei kabisa kuja sasa ila atakuja mara itakapowezekana. |
13 |
Kesheni, simameni imara katika imani, muwe hodari na wenye nguvu. |
14 |
Kila mfanyacho kifanyike kwa upendo. |
15 |
Ndugu, mnaifahamu jamaa ya Stefana; wao ni watu wa kwanza kabisa kuipokea imani ya Kikristo katika Akaya, na wamejitolea kuwatumikia watu wa Mungu. Ninawasihi ninyi ndugu zangu, |
16 |
muufuate uongozi wa watu kama hao, na uongozi wa kila mtu afanyaye kazi na kutumikia pamoja nao. |
17 |
Nafurahi sana kwamba Stefana, Fortunato na Akaiko wamefika; wamelijaza pengo lililokuwako kwa kutokuwako kwenu. |
18 |
Wameiburudisha roho yangu na yenu pia. Kwa hiyo inafaa kuwakumbuka watu wa namna hii. |
19 |
Makanisa yote ya Asia yanawasalimuni. Akula na Priskila pamoja na watu wote wa Mungu walio nyumbani mwao wanawasalimuni sana katika Bwana. |
20 |
Ndugu wote wanawasalimuni. Nanyi salimianeni kwa ishara ya mapendo ya Mungu. |
21 |
Mimi Paulo nawasalimuni, nikiandika kwa mkono wangu mwenyewe. |
22 |
Yeyote asiyempenda Bwana, na alaaniwe. MARANA THA--BWANA, njoo! |
23 |
Neema ya Bwana Yesu iwe nanyi. |
24 |
Mapendo yangu yawe kwenu katika kuungana na Kristo Yesu. |