Alice Walker
From Wikipedia
Alice Malsenior Walker (amezaliwa 9 Februari, 1944) ni mwandishi wa kike kutoka nchi ya Marekani. Aliandika hasa riwaya na mashairi yanayoonyesha hali ya Wamarekani-Waafrika. Anajulikana hasa kwa riwaya yake “Rangi ya Zambarau” (kwa Kiingereza: The Color Purple) iliyotolewa 1982. Mwaka wa 1983 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Pulitzer kwa ajili ya riwaya hiyo.