Tobias Asser
From Wikipedia
Tobias Michael Carel Asser (28 Aprili, 1838 – 29 Julai, 1913) alikuwa mwanasheria kutoka nchi ya Uholanzi. Alikuwa profesa wa sheria kwenye Chuo Kikuu cha Amsterdam. Mwaka wa 1899 na tena 1907 alikuwa mwakilishi wa Uholanzi kwenye mikutano ya amani iliyofanyika katika mji wa The Hague. Mwaka wa 1911, pamoja na Alfred Fried alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel kwa Amani.