Abushiri ibn Salim al-Harthi
From Wikipedia
Abushiri ibn Salim al-Harthi alikuwa kiongozi wa upinzani dhidi ya ukoloni wa Wajerumani katika maeneo ya Pangani na pwani la Tanzania mnamo 1889.
Alikuwa mwenye shamba ya miwa karibu na Pangani. Agosti 1889 alishiriki katika upinzani dhidi ya utawala wa Shirika la Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki akawa kiongozi.
Baada ya miezi ya mapambano alikamatwa na kunyongwa na Wajerumani tarehe 16 Desemba, 1889.