Bendera ya Iceland
From Wikipedia
Bendera ya Iceland imepatikana tangu mwaka 1915. Ina rangi ya buluu ikionyesha msalaba mweupe ndani yake. Ndani ya msalaba nyeupe kuna msalaba mwembamba zaidi nyekundu.
Muundo wa bendera ni ile ya bendera zote za Skandinavia zinazofuatamfano wa bendera ya kale ya Denmark inayoitwa Danebrog.
Rangi ya buluu inaikumbusha rangi ya anga juu ya Iceland.
Kwa ujumla inafanana mno na bendera ya Norway isipokuwa kwa kubadilishana rangi. Iceland ina uhusiano wa karibu sana na Norway tangu mwanzo wake.