Ernest Orlando Lawrence
From Wikipedia
Ernest Orlando Lawrence (8 Agosti, 1901 – 27 Agosti, 1958) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Marekani. Hasa alifanya utafiti wa fizikia ya kiini. Mwaka wa 1939 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia. Mwaka wa 1941 alifaulu kutenganisha isotopu za elementi ya urani.