Fritz Lipmann
From Wikipedia
Fritz Albert Lipmann (12 Juni, 1899 – 24 Julai, 1986) alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Ujerumani; baadaye alihamia Marekani. Hasa alichunguza vimeng’enya katika chembe hai vibadilishavyo chakula kuwa nishati. Mwaka wa 1953, pamoja na Hans Krebs alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.