Nyanda za Juu za Bie
From Wikipedia
Nyanda za Juu za Bie ziko kwenye kitovu cha nchi Angola. Zinapanda hadi ya kuwa na kimo cha 2,619 m juu ya UB.
Kutokana na kiasi kikubwa cha mvua kinachopatikana hapa eneo ni chanzo cha mito mingi muhimu ya Afrika ya Kusini na Afrika ya Kati.
[edit] Mito muhimu inayoanza Nyanda za Juu za Bie
- Kwanza (Cuanza) - inaelekea kaskazini - magharibi na kuishia Atlantiki
- Kasai inaelekea kaskazini na kuishia mto Kongo
- Kwango inaelekea kaskazini na kuishia kwenye mto Kasai ndani ya Kongo.
- Kwando (Cuando) - inaelekea kusini-mashariki na kuishia Zambezi
- Kubango-Okavango - inaelekea kusini halafu kusini-mashariki na kuishia Delta ya Okavango kwenye Kalahari
- Kunene (Cunene) - inaelekea kusini-magharibi na kuishia Atlantiki mpakani na Namibia.
- kuelekea magharibi ni mito midogo tu
- Zambezi ikitokea kaskazini inapita karibu na Nyanda za Juu za Bie na kupokea sehemu ya maji yake hapa.
Mji mkubwa katika eneo ni Huambo (zamani: Lisbon mpya)