Senegal
From Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: Un Peuple, Un But, Une Foi (Kifaransa: Taifa moja, Lengo moja, Imani moja) |
|||||
Wimbo wa taifa: Pincez Tous vos Koras, Frappez les Balafons' | |||||
Mji mkuu | Dakar |
||||
Mji mkubwa nchini | Dakar | ||||
Lugha rasmi | Kifaransa | ||||
Serikali
Rais
|
Jamhuri Abdoulaye Wade |
||||
Uhuru kutoka Ufaransa |
20 Juni, 1960 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
196,190 km² (ya 85) {{{percent_water}}} |
||||
Idadi ya watu - 2005 kadirio - 2005 sensa - Msongamano wa watu |
11,658,000 (ya 72) 11,658,000 56.7/km² (110) |
||||
Fedha | CFA Franc ({{{currency_code}}} ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
UTC (UTC+0) (UTC) |
||||
Intaneti TLD | .sn | ||||
Kodi ya simu | +221 |
Senegal ni nchi ya Afrika ya Magharibi upande wa kusini wa mto Senegal. Imepakana na Mauritania upande wa kaskazini, Mali upande wa mashariki, Guinea na Guinea-Bisau kwenye kusini na Bahari Atlantiki upande wa magharibi. Nchi ya Gambia iko ndani ya eneo la Senegal. Visiwa vya Cabo Verde viko 560 km mbele ya pwani la Senegal. Ilikuwa koloni ya Ufaransa hadi 1960.
[edit] Jiografia
Senegal ni nchi inayogusana na kanda ya Sahel na pia kanda ya Tropiki. Uso wa nchi ni hasa tambarare zinazopanda juu polepole kuelekea kusini mashariki. Sehemu za zinafikia 580 m juu ya UB. Kusini kabisa iko kasoko kubwa la Velingara.
Hali ya hewa ni ya kitropiki. Majira ya mvua ni hasa miezi ya Mei hadi Novemba.
[edit] Miji
Miji mikubwa ni Dakar (wakazi 1,998,635), Touba (wakazi 428,059), Thiès (wakazi 240,152), Rufisque (Wakazi 187.203), Kaolack (Wakazi 173,782), Mbour (Wakazi 170,699), Ziguinchor (Wakazi 162,436) na Saint-Louis (Wakazi 130.750). Karibu nusu ya watu huishi mjini.
[edit] Wakazi
Kuna wakazi milioni 11 na idadi kubwa ni chini ya umri wa miaka 20. Wameongezeka sana, mnamo mwaka 1985 idadi ilikuwa milioni 5 tu. Kikundi kikubwa nchini ni Wawolof (33%), halafu Waserer (20%), wengine Wafulani, Wadiola, Watukulur, Wamandingo, Wasoninké.
Theluthi mbili ya wakazi hawajui kusoma.
Walio wengi sana ni Waislamu Wasunni (94%); Wakristo Wakatoliki takriban 5%.
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad |Cote d'Ivoire | Djibouti | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia |
Makala hiyo kuhusu "Senegal" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Senegal kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |