Yesu
From Wikipedia
Yesu alikuwa Myahudi aliyeishi miaka 2000 iliyopita. Baadhi ya Wakristo wanamwamini yeye ndiye Mungu aliyechukua maumbile ya mwanadamu au kwa lugha nyingine Mwana wa Mungu. Wakristo wengine wanaamini kuwa yeye ni mtume wa pekee wa Mungu ila sio Mungu. Katika dini ya Uislamu, Yesu anajulikana kama Nabii Isa. Waislamu wanaamini kuwa yeye alikuwa ni nabii wa Mungu ila hakuwa mwana wa Mungu wala Mungu,
Waumini wa mafundisho yake ndio msingi wa Kanisa la Kikristo leo linalopatikana katika madhehebu mbalimbali duniani.
Maisha yake imekuwa msingi kwa ajili ya sikukuu mbalimbali inayosheherekewa katika nchi nyingi duniani. Taz. Krismasi (kuzaliwa kwake), Epifania (kuonekana kwake pia kubatizwa kwake), Majilio au Kwaresima (mateso yake), Ijumaa Kuu (kifo chake); Pasaka (kufufuka kwake).
[edit] Misingi ya ujuzi wetu juu yake
Yesu hakuacha maandiko yoyote. Habari zake zinapatikana hasa katika maandiko ya Agano Jipya.
[edit] Chimbuko nje ya Ukristo
Kuna habari fupi kuhusu Yesu katika maandiko ya waandishi Waroma, Wagiriki na Wayahudi. Habari hizi zinaangaliwa sana kwa sababu zimetungwa na watu wasiomwamini Yesu hawakuwa Wakristo na wafuasi wake. Kwa ujumla zinathebitisha ya kwamba Yesu alikuwepo, alikuwa na wafuasi huko Roma na ya kwamba awali Waroma hawakuelewa tofauti kati ya wafuasi wake na Wayahudi. Muhimu ni hasa:
1. Testimonium Flavanium: mtaalamu Myahudi Flavius Josephus aliandika mn. Mw. 90 b.K. kitabu cha „Antiquitates Judaicae“ (Habari za historia ya Kiyahudi) akitaja kifo cha „Yakobo ndugu wa Yesu“ (sura ya 20, 200).
2. Mwandishi Mroma Tacitus aliandika mn. Mw. 117 ya kwamba Kaisari Nero alishtaki kikundi cha “Chrestiani” ya kuwa wamechoma moto mji wa Roma. Aliongeza: “Mtu ambaye ni asili ya jina hili ni Chrestus aliyeuawa wakati wa Tiberio kwa amri ya Pontio Pilato” (Annales XV,44).
3. Mwandishi Mroma Sueton alimtaja “Chrestos” katika kitabu chake juu ya maisha ya Kaisari Claudius (25,4) ya kwamba huyu amesababisha fujo kati ya Wayahudi wa mji wa Roma hivyo Kaisari aliwafukuza mjini.
4. Gaius Plinius Caecilius Secundus alikuwa mwanasiasa Mroma aliacha barua kadhaa zinazotaja Wakristo mnamo mwaka 100 b.K. Alimwuliza Kaisari Traian jinsi ya kushughulika Wakristo waliokataa kutoa sadaka mbele ya sanamu za Kaisari.
[edit] Tazama pia:
- - Makala "Yesu Kristo": mafundisho ya Kikristo kuhusu Yesu
- - Makala "Isa": mafundisho ya Uislamu kuhusu Yesu