Mita
From Wikipedia
Mita ni kipimo cha urefu kimekuwa kipimo cha kimataifa. Neno limetokana na Kigiriki μέτρον/métron = kipimo, pia chombo cha kupimia.
Kutokana na maana hiyo "mita" inataja pia mitambo ya kupima maji, umeme na kadhalika. Hapo matumizi ya Kiswahili kinafanana na Kiingereza "meter".
Contents |
[edit] Mita ya asili
Mita imeundwa kama kipimo wakati wa mapinduzi ya Kifaransa mwaka 1793. Nia ilikuwa kumaliza vipimo vya kale kutokana na viungo vya mwili kama hatua, mkono, mguu na kadhalika. Vipimo hivi asilia vilitofautiana kila mahali; Ujerumani ilikuwa na na futi zaidi ya kumi katika mikoa na majimbo mbalimbali. "Mita" imeamuliwa ni sehemu moja kati ya sehemu milioni 40 za meridiani ya Paris (mstari kutoka ikweta hadi ncha ya kaskazini unaopita mji wa Paris).
Mita ya asili ilichongwa kama reli ya shaba baadaye ya platini ambayo ni metali ngumu sana.
Nchi zote duniani hutumia vipimo vya mita hata kama nchi mbalimbali bado hutumia vipimo vya asilia kufuatana na utamaduni wao. Kwa mfano nchi za mapokeo ya Kiingereza hupenda inchi na futi. Matumizi ya vipimo ya kale katika maisha ya kila siku si kizuizi kupeleka watu angani. Warusi bado wanapenda kipimo cha "verst" (mita 1066,8), Waamerika huhesabu "yard" (mita 0,9144) lakini wote walifaulu kurusha makombora angani - isipokuwa kwa kutumia vipimo vya mita.
[edit] Elezo ya mita leo
Tangu 1960 mita imepataniwa ni umbali wa njia inayotembelewa na nuru katika anga pasipo na hewa katika muda wa sekonde 1/299,792,458.
[edit] Sehemu ndogo na wingi za mita
Kiasi | Jina | Kifupi | Kiasi | Jina | Kifupi | |
---|---|---|---|---|---|---|
100 | mita | m | ||||
10–1 | desimita | dm | 101 | dekamita | dam | |
10–2 | sentimita | cm | 102 | hektomita | hm | |
10–3 | millimita | mm | 103 | kilomita | km | |
10–6 | mikromita | µm | 106 | megamita | Mm | |
10–9 | nanomita | nm | 109 | gigamita | Gm | |
10–12 | pikomita | pm | 1012 | teramita | Tm | |
10–15 | femtomita | fm | 1015 | petamita | Pm | |
10–18 | attomita | am | 1018 | examita | Em | |
10–21 | zeptomita | zm | 1021 | zettamita | Zm | |
10–24 | yoktomita | ym | 1024 | yottamita | Ym |
[edit] Vipimo vya kawaida:
Kilomita (km) : Kilomita moja ni mita 1000
Sentimita (cm): Sentimita ni sehemu ya mia ya mita; mita ina sentimita 100.
Millimita (mm): Millimita ni sehemu ya kumi ya sentimita moja; sentimita ina millimita kumi, mita ina millimita elfu moja.