Thomas Aquinas Mtakatifu
From Wikipedia
Thomas Aquinas Mtakatifu (takriban 1224 – 7 Machi 1274) alikuwa mwanateolojia kutoka nchi ya Italia. Alikuwa mtawa ndani ya Shirika la Wadominikani. Alichunguza hasa mawazo ya mwanafalsafa Mgiriki Aristoteli. Pia anajulikana sana kwa vitabu vyake “Jumla ya Teolojia” (kwa Kilatini Summa theologiae) na “Jumla dhidi ya Wapagani” (kwa Kilatini Summa contra gentiles). Alitangazwa kuwa mtakatifu 18 Julai 1323. Sikukuu yake ni 28 Januari.